Vita vyake vya mwisho bado havijapiganwa. Kitabu cha Ufunuo kinaeleza mapatano na baadhi ya watetezi wenye nguvu ambao hatimaye wanawaangamiza watesi wa Israeli na kuiasisi katika usalama wa milele. Washirika hao wanapewa jina lenye fumbo “wafalme wa mashariki” katika Ufunuo 16:12. Kwa hakika wanaingilia kati ili kuwakomboa Israeli wakati wa vita vya Har–Magedoni, vinavyofafanuliwa katika Biblia kama pambano la mwisho litakalotokea kwenye sayari hii. Mataifa yote yatahusika katika vita hivi, lakini Israeli pekee atakuwa mshindi. Madhumuni yetu katika utafiti huu ni kujibu maswali kadhaa.
Vita hivyo vya mwisho vya Har–Magedoni ni nini? Je, nchi zote za ulimwengu zinawezaje kuhusika katika hilo? Inawezekanaje kwa kundi moja tu, watu wa Israeli, kunusurika kwenye maangamizi haya makubwa? Ni wafalme gani wa ajabu wa mashariki wanaoleta ushindi wake Israeli? Na hatimaye, Israeli wakombolewaje kutoka kwa adui zake kwa kukauka kwa Mto Frati, kama inavyofafanuliwa katika Ufunuo 16:12? Kwanza kabisa, tunahitaji kujua kama taifa la sasa la Israeli ni Israeli ile ile ambayo imetajwa katika kitabu cha Ufunuo kama watu wa Mungu. Baadhi ya unabii wa kushangaza sana unapatikana katika kitabu hicho, mwingi kati yao ukihusu kuokoa kundi la masalia wa vita la wafuasi waaminifu wa Yesu Kristo. Wafuasi hao wakati mwingine huitwa “kabila za Israeli” na wananenwa katika muktadha wa desturi za Kiyahudi. Je, hilo lamaanisha kwamba taifa halisi la Israeli—lile linalopigana kwa vifaru na mabomu—litajigeuza kabisa na kuwa Wakristo?
Je, wataweka kando matamanio yao ya Kizayuni ya kuwaua washambuliaji wao na kuunga mkono kanuni za amani za Mahubiri ya Mlimani—yale ya kumpenda adui na kumgeuzia shavu jingine? Mamilioni ya wanafunzi wa Biblia wanaamini kwamba ni lazima wongofu wa namna hiyo wenye kuvutia utukie ili unabii wa Biblia utimizwe. Wanaegemeza imani yao juu ya unabii unaopatikana katika Yeremia, Ezekieli, Isaya, n.k., kuhusiana na urejeshwaji wa Israeli na ushindi wa mwisho. Je, wako sahihi? Ni kweli kwamba manabii walitoa mifano mizuri ya wakati ujao wa Israeli na kuandika ahadi nyingi kuhusu mamlaka yake juu ya mataifa mengine. Lakini je, Israeli wa Agano la Kale ni Israeli yule yule wa kitabu cha Ufunuo? Je, ahadi hizo hazikuwa na masharti wala kubatilishwa? Je, wazao halisi wa Abrahamu wa kimwili watamgeukia Masihi, warejeshwe kuwa taifa, na kuokolewa kama watu?
Baadhi ya wafafanuzi wa leo wamefanya makosa kutumia unabii huo wa urejesho kwa mkusanyiko fulani wa siku zijazo wa Israeli. Wanakataa kuona kwamba urejesho ulionenwa na Isaya na Yeremia tayari umekwisha tukia. Hakuna wakati wala nafasi ya kuandika hapa sehemu ya vitisho vya wazi vya kukataliwa vilivyotolewa kwa Israeli. Tena na tena Mungu alitoa maonyo kama haya: “Ukienda mbele zangu … kufanya hayo yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, ndipo nitakapokifanya imara kiti cha ufalme wako juu ya Israeli milele; …. Bali mkighairi, mkaacha kunifuata, ninyi na watoto wenu, msizishike sheria zangu na amri zangu,… basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote.” (1 Wafalme 9:4-7).
Hatimaye, kama ilivyosimuliwa kupitia nabii Danieli, Mungu alitenga kipindi cha rehema cha miaka 490 kwa Wayahudi kuona kile ambacho wangefanya kuhusu Masihi (Danieli 9:24). Kipindi hicho cha wakati wa kinabii cha majuma 70 (siku kwa mwaka, Ezekieli 4:6) kilianza kwa kutolewa kwa amri ya kurejesha na kujenga Yerusalemu (amri ya Artashasta mwaka 457 KK, Ezra 7:11) na kumalizika mwaka 34 BK. Katika mwaka huo huo injili ilianza kwenda kwa Mataifa, Stefano alipigwa mawe, na Paulo akatoka ili kuanza huduma yake ya kipekee kwa wasio Wayahudi. Tukio hilo liliashiria utengano rasmi na wa mwisho wa Israeli kutoka katika uhusiano wao wa agano.
Yesu alikuwa amewaeleza viongozi wa Kiyahudi kwa lugha iliyo wazi kabisa kwamba kumkataa kwao kungetia muhuri kukataliwa kwao wenyewe kama watoto wa ufalme. “Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, na kupewa taifa lenye kuzaa matunda yake” (Mathayo 21:43). Hakuna siri kwa nini mamia ya ahadi mahususi za Agano la Kale hazikutimizwa kamwe kwa Israeli. Walishindwa kabisa kutimiza masharti ya utii. Vinginevyo, wangerithi dunia, wangekombolewa kutoka kwa adui zao wote, na kufanya Yerusalemu kuwa kitovu cha ibada cha mataifa yote.
Kwa kutumia kanuni hii kwa Maandiko ya Agano la Kale hakuna kabisa mkanganyiko kuhusu nafasi ya Israeli katika unabii na historia. Ahadi zote tukufu zililenga hasa baraka za papo hapo ambazo Mungu alitaka kulipatia taifa. Lakini katika maana ya pili zilielekeza mbele kwenye utimizo mkubwa zaidi wa kiroho katika wigo wa ulimwengu wote. Ingawa utimilifu wa ndani kama taifa ulishindwa pale Israeli iliposhindwa kuwa waaminifu, ahadi hazikubatilishwa au kuondolewa. Zitainuliwa, lakini kwa lile “taifa” ambalo Yesu alisema lazima lichukue mahali pa Wayahudi kama wapokeaji wa ufalme. Ni taifa na watu gani hao? Agano Jipya limejaa taarifa za wazi zaidi kuhusu Israeli mpya ni nani.
Petro anafafanua wale “ambao zamani walikuwa si taifa, bali sasa ni watu wa Mungu” kwa maneno haya: “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu; mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu” (1 Petro 2:9, 10). Hapa kuna taifa jipya linalochukua nafasi ya taifa la Israeli. Watu wa Mataifa ambao watampokea Masihi wa kweli sasa wanaingia katika Agano Jipya, lililoidhinishwa kwa damu ya msalaba, na kuwa Israeli wa kweli wa kiroho wa Mungu. Wale ambao hawakuwa watu wa Mungu wanakuwa “taifa takatifu” Lake.
Je, watapata ahadi zilezile walizopewa wazao wa Ibrahimu? Kwa hakika, Biblia inasema kwamba wanahesabiwa kuwa uzao halisi wa Ibrahimu. “Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi” (Wagalatia 3:29). Paulo anaiweka wazi zaidi katika Warumi 9:8. "Wale walio watoto wa mwili sio watoto wa Mungu; lakini watoto wa ahadi wamehesabiwa kuwa wazao." Tena, Paulo aliandika, “Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu; wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili; bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani; na tohara ni ya moyo” (Warumi 2:28, 29).
Tambua kwamba Israeli wa kweli watakuwa na sifa ya tohara ya moyo na si ya mwili. Tohara ya moyo ni nini? “Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.” (Wakolosai 2:11). Usikose umuhimu wa maandishi hayo. Jinsi Agano la Kale lilivyowakilishwa kwa kukatwa kwa nyama ya mwilini, vivyo hivyo Agano Jipya lingeonyeshwa kwa kukatwa kwa asili ya kimwili ya dhambi. Kwa maneno mengine, wote wanaomkubali Kristo na kuzaliwa mara ya pili ndio waliotahiriwa kweli na ndio Wayahudi pekee wa kweli. Na kulingana na Paulo wao pia watarithi ahadi zilizofanywa kwa Ibrahimu.
Baada ya kusulubishwa kwa Kristo, hakuna ishara hata moja kwamba Wayahudi wa kimwili walipewa kutambuliwa kama watoto wa Mungu. Ni kweli kwamba mlango bado ulikuwa wazi kupitia mahubiri ya mitume hadi mwaka wa 34 BK, mwisho wa unabii wa Danieli wa majuma sabini. Lakini tangu wakati huo na kuendelea hakuna kutambuliwa kunakotolewa kwa Israeli kama taifa. Israeli tangu sasa na kuendelea ni watu wa Mungu, kujumuisha wale wote wanaomkubali Mwokozi, wawe Wayahudi au Wamataifa. Matumizi ya lugha ya picha na istilahi za Agano la Kale bado zinatumika, hasa katika kitabu cha Ufunuo, lakini Israeli sasa ni kanisa.
Kwa hiyo tunaweza kuona kwamba hakukuwa na kushindwa kwa ahadi hata kidogo. Walihamishiwa kuwa Israeli wa kweli wa kiroho, ambalo ni kanisa, linalojumuisha na waamini wote wa kweli katika Kristo. Na mambo yatakayotokea kwa kanisa kiroho yalifananishwa na yale yaliyowapata Waisraeli wa kale katika maana halisi. Hebu tuangalie mfano rahisi wa kanuni hii katika utendaji. Katikati ya taswira ya Ezekieli juu ya ushindi wa Israeli dhidi ya adui zao na ushawishi juu ya mataifa, alianza kufafanua hekalu zuri sana ambalo lingejengwa. Sura kadha wa kadha (40-48) zimetolewa kwa vipimo sahihi na uteuzi wa hekalu hilo.
Hata hivyo hekalu halijawahi kujengwa. Manabii wengine walirejelea mpango wa kujenga au kurejesha hekalu kama hilo. Amosi alitabiri, “Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobomoka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale” (Amosi 9:11). Wafasiri wengi wa leo hutumia ahadi hii kwa ujenzi wa baadaye wa hekalu halisi. Lakini kanuni ya Biblia ni kwamba kuna utimizo upili, wa ulimwenguni pote ambao si wa kimwili, bali wa kiroho. Agano Jipya linathibitisha hili kwa kueleza jinsi unabii wa Amosi ulivyotimizwa. “Simeoni ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake.
Na maneno ya manabii yapatana na hayo, kama ilivyoandikwa, Baada ya mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha” (Matendo 15:14-16). Tafadhali angalia jinsi unabii wa Agano la Kale unavyotumika kwa kanisa lililo hai! Hekalu la kimwili sasa limekuwa hekalu la kiroho la kanisa, linaloundwa na Mataifa na waumini wote wa kweli. Hakuna mtu anayepaswa kutafuta sasa hekalu lolote lililorejeshwa, halisi ambalo linapaswa kujengwa. Mwili wa kanisa la Kristo sasa ni hekalu (1 Wakorintho 3:16), na sisi ni “mawe yaliyo hai” ya hiyo “nyumba ya kiroho” (1 Petro 2:5).
Wengine wamechanganyikiwa kwa sababu sehemu kubwa ya istilahi za Agano la Kale zimehamishwa hadi katika maelezo ya Agano Jipya ya kanisa— maneno kama ufalme, taifa, Israeli, hekalu, Yerusalemu, Sayuni, makabila ya Israeli, nk. Hata Kristo aliwaambia Mafarisayo, Je! “Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, (Israeli halisi) na kupewa taifa (Israeli wa kiroho) lenye kuzaa matunda yake” (Mathayo 21:43). Hii ni sababu moja ya waamini wa unabii wa wakati ujao katika utimizo wa kimwili na waamini wengine kwamba kitabu cha Ufunuo kinahusu Myahudi halisi katika Israeli ya leo. Lakini hakuna sababu ya mkanganyiko kama huo. Ufafanuzi huo ulikuwa umetolewa kwa uwazi katika sehemu nyingi sana kiasi kwamba mwandishi wa Agano Jipya alidhani kwamba wote walikuwa wanajua kwamba kanisa sasa lilichukua nafasi ya taifa la Israeli.
Kwa historia hii tumejitayarisha kujifunza somo la Har–Magedoni. Mgogoro huo wa mwisho wa ulimwengu unafungamana kwa karibu na mambo ambayo tumetoka tu kusema kuhusu Israeli wa kiroho na matumizi ya pili ya unabii. Kuna ulinganifu wenye kustaajabisha zaidi kati ya yale yaliyoipata Israeli ya kale na matukio yanayohusu Israeli wa kiroho katika kitabu cha Ufunuo. Utagundua kwamba watu wa Mungu walikuwa na uzoefu karibu sawa katika Agano la Kale na Agano Jipya. Walilazimishwa kuabudu sanamu na waliokolewa na mtu kutoka mashariki ambaye aliukausha mto Frati ili kuwakomboa.
Ndani ya muhtasari huu mpana kuna mengi ya ufanano mwingine wa kustaajabisha kati ya Israeli ya Kale Israeli ya Kiroho Yer. 50:33,34 Kuteswa na Babeli Ufu. 17:6 Dan. 3:13 Kulazimishwa kuabudu sanamu Ufu. 13:15 Dan. 4:30 Mji Uitwao “Babeli mkuu” Ufu. 17:5 Yer. 51:13,14 Babeli wakaa juu ya maji mengi Ufu. 17:1 Isa. 44:27, 28 Kuokolewa—Mto Frati wakauka Ufu. 16:12 Yer. 51:6-8 Watu waitwa kutoka Babeli Ufu. 18:4 Isa. 45:1 Mkombozi wao aitwa mpakwa mafuta Dan. 9:25 Isa. 41:2, 25 Wakombozi wote watokea mashariki Math. 24:27,Ufu. 7:2 Waisraeli wawili—moja wa mwili na mwingine wa kiroho. Ni wazi kwamba kanisa—watu wa Mungu wa siku za mwisho—watateswa na kutishwa kwa kifo kama ilivyokuwa kwa Israeli ya kale.
Katika kitabu cha Ufunuo wanakombolewa kutoka katika Babeli ya kiroho kwa kuhusianisha na vita vya Har–Magedoni. “Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua. Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi…… Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.” (Ufunuo 16:12-16). Aya hizi zimejaa maana kubwa.
Yanaonyesha kwamba nguvu tatu kuu zitatumiwa na Shetani katika kuandaa njia kwa ajili ya Har– Magedoni. Hizo tatu—mnyama, joka na nabii wa uongo—wanachochea mamlaka za kisiasa za dunia kushiriki katika vita hivyo. Ni dhahiri kwamba hizo nguvu tatu ni mamlaka za kidini, kwa kiasi katika madai yao, kwa sababu zinafanya miujiza ili kuzivutia serikali za dunia. Miujiza inatenda kazi tu ndani ya ulimwengu wa dini. Wakati na nafasi hazituruhusu kutoa ushahidi wote wa kibiblia kuonyesha jinsi nguvu hizi tatu zinavyojumuisha aina zote za leo za dini bandia. Zikikataa mamlaka ya sheria ya Mungu na kuchagua mapokeo rahisi ya kanuni za ibada ya kipagani, mifumo hii ya kidini iliyounganishwa itatumia uvutano mkubwa katika kuuvuta ulimwengu wote kwenye vita vya Har–Magedoni.
Har–Magedoni ni kilele tu cha programu ya miaka 6,000 ya Shetani ili kuwazibiti watu wa Mungu wasiokolewe. Akiwa kama adui, ambaye kwa ubinafsi wake mwenyewe kulimfanya afukuzwe mbinguni, Shetani alitangaza kusudi lake la kumwangusha Mungu na kuchukua serikali Yake ya ufalme wote. Sikiliza majivuno yake katika Isaya 14:13, 14 “Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.
Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu…” Dai hili la kushangaza la Shetani linafichua kiini cha mpango wake wa kujiweka mahali pa Mungu. Ili kupindua ibada ya watu wa Mungu na kuwageuzia kwake mwenyewe ingeonekana kuwa jambo la kawaida na la lazima kwa Shetani kujenga mvuto wake kwenye dini. Akifanya kazi katika vazi la mifumo ya kidini ya uongo na ibada ya uongo, amesuka mchanganyiko wa werevu wa ukweli na makosa katika vizazi vyote. Udanganyifu wake mkuu utatokea wakati wa mwisho atakapofanya kazi kupitia kwa mamlaka ya mnyama ili kutekeleza alama ya uaminifu kwa kila mtu. Wale wanaokataa alama hiyo watahukumiwa kifo, na hivyo, kizuizi cha mwisho kitaondolewa kwa Shetani kudai viumbe vyote kuwa wafuasi wake. Ndivyo unavyosomeka msingi wa mbinu ya Shetani.
Hapo ndipo Mungu atawakusanya watu wake, mkutano wake. Mlima Sayuni ni mahali pa usalama. Shetani anataka kuharibu kusanyiko au watu wa Mungu. Angepenya kwa wateule hasa kwa madanganyo yake na kuwachukua, pamoja na kiti cha enzi cha Mungu. Mtunga-zaburi alisema, “Mwimbieni Bwana akaaye Sayuni” (Zaburi 9:11). Hapo awali, Sayuni ilikuwa mahali palipokusudiwa ambapo hekalu lilikuwa, katika sehemu ya kaskazini ya Yerusalemu. Baadaye, lilikuja kujulikana kuwa ishara ya mji wa Yerusalemu. Pia inatumika katika Maandiko yote kwa watu wote wa Mungu. Lakini baada ya Wayahudi kumkataa Yesu neno Sayuni lilikuja kuwa ishara ya kanisa. Hivyo katika Agano Jipya haitambuliki tena mahali halisi duniani, bali watu—watu wa kanisa waliotawanyika ulimwenguni kote, au pengine mahali pa kiroho pa uwepo na ulinzi wa Mungu.
Katika Biblia yote Mungu anaelezewa kuwa anawavuta au kuwakusanya watu wake Sayuni ambapo wanaweza kuwa salama pamoja Naye. “Pigeni tarumbeta katika Sayuni,… Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko” (Yoeli 2:15, 16). “Kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka,” (Yoeli 2:32). Katika Ufunuo 14:1 waliokombolewa wanaonyeshwa wakiwa wamekombolewa kutoka kwa mamlaka ya mnyama wa sura iliyotangulia na wako salama katika Mlima Sayuni. “Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.” Lakini wakati Mungu anapanga kusanyiko la watu Wake Kwake katika Sayuni, Shetani pia ana programu ya kukusanya.
Ni mkusanyiko wa majeshi yake kwa ajili ya Har–Magedoni. “Hizo ndizo roho za mashetani…… kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi…… Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, HarMagedoni.” (Ufunuo 16:14, 16) Kusanyiko hili ni la kupinga kusanyiko la Mungu la watakatifu Wake kwenye mlima Sayuni. Yoeli pia anazungumza juu ya kusanyiko hilo hilo; “Fanyeni haraka, mje, enyi mataifa yote, wa pande zote, jikusanyeni pamoja…… Mataifa …… wakapande juu katika bonde la Yehoshafau…… Naye Bwana atanguruma toka Sayuni…… lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli” (Yoeli 3:11, 12, 16).
Haya ni maelezo mengine ya pambano hilo la mwisho liitwalo Har–Magedoni. Bonde la Yehoshafati ni utambulisho mwingine wa mahali pa vita. Itahusisha kila taifa duniani. Neno “mataifa/wapagani” ni neno linalowafafanua wale ambao si watu wa Mungu. Shetani atawaongoza wafalme wa dunia na watu wote waovu ili kuwapinga watakatifu waaminifu wa Mungu. Bwana atahusika katika vita (“Bwana atanguruma toka Sayuni”), kwa sababu anawapigania watu wake. Kimsingi, ni pambano kubwa kati ya Kristo na Shetani huku wafuasi wa pande zote mbili wakihusika. Hapa ndipo tunapofikia kiini cha somo. Mstari huo unakazia neno la Kiebrania la Har–Magedoni.
Kwa dhahiri neno hilo linatokana na neno la Kiebrania “har moed,” linalomaanisha “mlima wa mkutano” au “mlima wa kusanyiko.” Unaona hii inatupeleka wapi? Neno hilohilo (har moed) lilitumiwa na Shetani aliposema, “Nitaketi juu ya mlima wa mkutano.” Hii inaunganisha vita vya Har–Magedoni na tishio la awali la Shetani la kuvamia na kuharibu kusanyiko la Mungu—katika Mlima Sayuni. Na jaribio la mwisho la yule mwovu kutekeleza tishio lake linafikia matukio ya mwisho kabisa ya dunia hii. Yohana wa Ufunuo alilielezea ndani ya pigo la sita. Aliona roho chafu zikitoka kuwaendea wafalme wa dunia, zikifanya miujiza na kuwakusanya kwenye Har–Magedoni. Hizi ni nguvu za kidini zinazofanya kazi juu ya watawala wa kisiasa na kuwavuta waangamize waaminifu wa Mungu.
Ukitaka kusoma simulizi la kusisimua la utendaji wa Mungu katika Har–Magedoni, soma Ufunuo 19. “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wakweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita…… Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi…… naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi” (Ufunuo 19:11- 15). Mambo kadhaa yanajitokeza katika picha hii ya mfano ya Kristo na kuja kwake mara ya pili. Majeshi ya mbinguni kufanya vita na "kuwapiga mataifa" (Fungu la 15). Haya ni mataifa ambayo yalichochewa na zile roho chafu za Ufunuo 16:14. Kristo anashinda katika pambano hili la Har–Magedoni.
Tambua kwamba vita hivi vinafafanuliwa kuwa ni kukanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya Mungu. Katika Ufunuo 15:1 mapigo saba ya mwisho yametajwa kuwa “ghadhabu ya Mungu.” Kwa kuwa vita vya Har–Magedoni vimewekwa chini ya pigo la sita, na mapigo yanaitwa ghadhabu ya Mungu; na kwa kuwa jeshi la Kristo hufanya vita kwa kukanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya Mungu, tunapaswa kukata kauli kwamba Ufunuo 19 ndiyo picha halisi ya vita vya Har–Magedoni. Kwa bahati mbaya, vitasa vya ghadhabu ya Mungu vilimwagwa juu ya dunia nzima. “Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.” (Ufunuo 16:1). Hii ndiyo sababu mataifa yote yanahusika katika Har–Magedoni. Wema na waovu wa ulimwengu wote wataletwa kwenye vita hiyo. Kwa kuwa watu wa Mungu wametawanyika katika kila nchi, dunia nzima inasemwa kuwa inaathiriwa na mapigo, ambayo mojawapo ni Har–Magedoni.
Koreshi alikuja kutoka mashariki na kuteka Babeli kwa kuugeuza mkondo wa maji ya Mto Frati, hivyo akapata njia ya kuingia chini ya malango ya maji ya mifereji hiyo. Mungu aliuambia Babeli, “Nami nitaikausha mito yako. ... Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake… ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa” (Isaya 44:27; 45:1). Mungu “alimwinua mwenye haki (Koreshi) kutoka mashariki” (Isaya 41:2). Koreshi anatajwa na Mungu kuwa “mtiwa-mafuta” na “mwenye haki.” Kulingana na kanuni ya tafsiri, maelezo halisi katika Agano la Kale lazima yatumike katika maana ya kiroho wakati wa mwisho. Hivyo, tunasoma katika kitabu cha Ufunuo kuhusu Israeli wa kiroho (kanisa) wakiteswa na ''Babeli Mkuu (Ufunuo 17:5, 6).
Babeli hii si ufalme wa kimwili bali ni mfumo wa dini bandia unaoendeshwa na Shetani. Hatimaye watu wa Mungu wakombolewa kutoka kwa nguvu za Babeli wa kiroho kwa kukauka kwa maji ya mto Frati. “Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua” (Ufunuo 16:12). Mfanano wa kushangaza kwa yale yaliyotukia katika Agano la Kale ni dhahiri, lakini lazima tukumbuke kwamba matumizi upili hayawezi kuwa halisi bali kiroho. Utimizo wa papo hapo daima huwa ni halisi na wa ndani ya taifa husika, lakini utimizo wa siku ya mwisho unachukua ulimwengu pote na una matumizi ya kiroho pekee. Kwa hiyo, hatutarajii Koreshi halisi kukausha mto halisi ili kuwakomboa Waisraeli wa kimwili.
Tayari tumekwishagundua kwamba watu wote wa kweli wa Mungu ni Waisraeli wa kiroho. Sasa maji yanawakilisha nini? “Yale maji uliyoyaona ... ni watu, na makutano, na mataifa, na lugha” (Ufunuo 17:15). Katika sura hii Babeli Mkuu anaonyeshwa akiwa ameketi “juu ya maji mengi” (Ufunuo 17:1). Maji yanatambulika kama watu na mataifa yanayomtegemeza yule kahaba mkuu wa Babeli (dini ya uongo) awatesaye watakatifu wa kweli (Ufunuo 17:6). Kwa hiyo kukauka kwa maji kunawakilisha kuondolewa kwa msaada wa wale watu waliokuwa wafuasi wa mfumo wa Babeli.
Hili ni mojawapo ya matukio ya mwisho yanayotokea kabla tu ya kuja kwa Kristo. Watu wanatambua kwamba wamedanganywa, na kwa hasira wanageukana. Zekaria aeleza kile kinachotukia chini ya pigo hilo la saba Har–Magedoni inapofikia upeo wayo. “Na hii ndiyo tauni, ambayo Bwana atawapiga watu wote waliofanya vita juu ya Yerusalemu (watu wa Mungu)……Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba mashaka makubwa yatokayo kwa Bwana yatakuwa kati yao; na kila mmoja wao atakamata mkono wa jirani yake, na mkono wake utainuliwa ili kushindana na mkono wa jirani yake” (Zekaria 14:12, 13).
Yohana alieleza tukio hilo hivi, “Hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.” (Ufunuo 17:16). Jinsi Frati halisi katika Babeli ya kale ulivyogeuzwa kutoka kuwa mali na kuwa njia ya kuuangamiza mji, ndivyo maji yategemezayo (watu) ya Babeli wa kiroho yanageuka kuwa njia ya uangamivu wake. Kukauka huku kwa nguvu ya msaada kunatayarisha njia kwa ajili ya “wafalme wa mashariki” kuja na kuwakomboa watu wa Mungu kutoka mkononi mwa Babeli.
Hii ndiyo sababu pande mbili za kaskazini na mashariki zinatumika katika Biblia kama makao ya Mungu. “Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai” (Ufunuo 7:2). Kristo atarudi katika dunia hii kutokea mashariki. “Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.” (Mathayo 24:27). "Wafalme wa mashariki" ni sawa kabisa na majeshi ya mbinguni katika Ufunuo 19 ambao wanamshinda “huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao” (Fungu la 19).
Utukufu wa Mungu ulielezwa na Ezekieli kuwa ulitokea mashariki. “Kisha akanileta mpaka langoni, yaani, lango lile lielekealo upande wa mashariki; 2 na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulitokea kwa njia ya mashariki…nayo nchi iling'aa kwa utukufu wake” (Ezekieli 43:1, 2). Yohana alifunua ukuu wa kustaajabisha wa Kristo akiongoza majeshi ya mbinguni kufanya vita. “Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe…… Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana.” (Ufunuo 19:14, 16). Ni mandhari iliyoje! “Wafalme wa mashariki” wanapanda dhidi ya “wafalme wa dunia” na wa ulimwengu wote.
Babeli wa kiroho na majeshi yote yaliyomfuata yataangamizwa na Mfalme wa wafalme ambaye atatawala milele na milele. Koreshi, mtu tokea mashariki, aliyeokoa Israeli ya kimwili kutoka mikononi mwa Babeli ya kale, alikuwa mfano wa “wafalme wa mashariki” ambao wangeokoa Israeli wa kiroho kutoka Babeli. Vile Koreshi alivyoitwa “mtiwa-mafuta” na “mtu wa haki,” ndivyo Yesu alivyoitwa kwa majina yaleyale. Kufikia sasa twaweza kuhitimisha kwa urahisi kwamba ujio wa pili wa Kristo ndio tumaini pekee la Israeli. Mungu na Kristo, Wafalme wa kweli wa mashariki, watatokeza kwenye ulimwengu huu katika usiku wa manane wa mwisho wa mwanadamu. Pale alama ya mnyama inapotekelezwa na kila mpango wa mwanadamu wa kuokoka utakapokomeshwa, waaminifu wa Mungu watatwaliwa kutoka katika kifo hakika.
Lakini yeyote asiendelee kung’ang’ania tumaini tupu kwamba Israeli hii ina uhusiano wowote na watu wa kweli wa Mungu. Mahali pao pamechukuliwa na taifa lingine, tiifu na aminifu—ambao wametoka katika kila kabila, lugha na watu. Hao ndio Israeli wa kweli. Kamwe hawatachukua silaha kupigana na mtu yeyote. Wataishi kama Yesu alivyoishi na kuchagua kifo mbele ya kuvunjiwa heshima. Muungano dhaifu wa amani uliotiwa saini Machi 26, 1979, ungekuwa chini ya ubatili, hata ikiwa taifa la Israeli bado lingekuwa watu wateule wa Mungu. Miaka mingi iliyopita muungano kama huo ulifanywa na Mungu akauthamini kwa maneno haya: “Basi, nguvu za Farao zitakuwa aibu yenu, na kutumainia kivuli cha Misri kutakuwa kufadhaika kwenu…… Kwa maana Misri huwasaidia bure, bila faida…… Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana” (Isaya 30:3, 7, 9).
Mungu anatafuta wale wanaotumainia haki badala ya nguvu. Kwa hao atawaokoa kutoka kwa kila adui kupitia kwa wafalme washindi wa mashariki. Hebu macho yetu yasitazame kule kwenye nchi za mafuta na fitina za kisiasa za mashariki na kuziweka mahali pa anga ya mashariki, kwa sababu ni kutoka huko kwamba washirika wetu wa kweli watatuokoa.
Na kwa nini vazi ni muhimu kwa wale wanaomngoja Yesu aje? Ufunuo 19:7, 8 inatoa jibu hili la kushangaza: “Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing'arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.” Kama mwanga wa kutafuta maneno haya yanaangazia maana ya Ufunuo 16:15. Mavazi hayo yanaashiria haki ya Kristo ambayo kila mtu anapaswa kuvikwa ambaye angekuwa tayari kukutana na Bwana. Vita vya Har–Magedoni vitapiganwa juu ya suala la haki ya Kristo.
Ni wale tu ambao wameamini kabisa faida za maisha ya Kristo yasiyo na dhambi na kifo cha upatanisho wanaweza kushinda pamoja Naye dhidi ya nguvu za uovu. “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa” (Ufunuo 12:11). Hapa kuna muungano wa ushindi ambao hatimaye utamtupa chini mshitaki wa ndugu. Watakatifu walipata ushindi kwa imani yao rahisi katika utoshelevu wa msalaba. Hakuna imani katika mwili. Hakuna imani katika matendo ya sheria ya kujihesabia haki. Haki Yake pekee itakasayo na kutia nguvu. Kwa hiyo muungano huo ni wa aina tatu: 1) imani katika haki ya Yesu, 2) kushiriki bila woga “neno la ushuhuda wao,” na 3) “hawakupenda maisha yao hata kufa.” Kwa maneno mengine, wangependelea kufa kuliko dhambi.
Pale msalaba umefanya hivyo kwa mtu, anaweza kuokoka katika mashambulizi yote magumu ya Har-Magedoni nyingi. Mapepo, malaika walioanguka na Shetani mwenyewe lazima wakimbie kwa hofu mbele ya mamlaka ya maisha yaliyojazwa na Kristo. Imani ya kweli huzaa utii kamili, na kwa hiyo, haki ya kweli kwa imani inajumuisha utakaso pamoja na kuhesabiwa haki. Wale ambao wangekubali kufa badala ya kutomtii Mungu ndio pekee watakaokataa alama ya mnyama. Umati wa watu, wenye kitu kidogo kuliko haki ya kweli kwa imani, hawatahisi kwamba utii kwa amri zote unastahili kufa.
Wengi watafikiri kwamba utii wa Kristo umehesabiwa kwao, na kwa hiyo hawahitaji kuhangaikia matendo ya sheria. Watu kama hao hawaelewi injili kamili. Ni “uweza wa Mungu uletao wokovu”—sio tu uweza wa kusamehe, bali pia uweza wa kulinda. Hatujaokolewa tu kutoka kwa hatia ya dhambi, bali pia kutoka kwenye dhambi yenyewe. Kwa hiyo Har–Magedoni na maandalizi ya kukutana na Kristo yanalenga uhusiano binafsi na Mwokozi. Wakiwa wamevikwa silaha za haki Yake, watakatifu watashinda hata mbele ya amri ya kifo.
Kama huna uhakikisho mtamu wa ulinzi huo wa kiroho sasa, vaa vazi Lake wakati huu. Likiwa limefumwa katika kitanzi cha mbinguni, halina uzi wa kubuni wa kibinadamu. Likivunja mamlaka ya dhambi katika maisha, linatoa haki na uweza wa maisha ya Kristo na kifo cha upatanisho. Huu na uwe uzoefu wako leo. Tutembelee katika www.amazingfacts.org Au Piga 800-538-7275. Usikose kozi yetu ya bure ya Unabii wa Biblia itolewayo hewani kupitia… www.bibleuniverse.com Jiunge leo na upanue maarifa yako!